Image
Image

News Alert:Watu 50 mkoani Rukwa wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kufanya vitendo vya ujangili.


Polisi Mkoani Rukwa inawashikilia watu 50 kwa tuhuma za kufanya vitendo vya ujangili, kufuatia msako mkali uliofanywa kwa ushirikiano na kikosi kazi cha taifa.
Katika msako huo wa wiki mbili pia zimekamatwa bunduki 48 ikiwemo bunduki aina ya AK 47, bastola tano pamoja na risasi mbalimbali zaidi ya 760, zilizokuwa zikitumika katika  ujangili na uhalifu mwingine kwenye pori la akiba la Lwafi Wilayani Nkasi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Bwana  JACOB MWARUANDA, akizungumza Mjini Namanyere Wilayani Nkasi amesema licha ya kukamatwa kwa bunduki na risasi hizo,pia zimepatikana nyara za serikali ikiwa ni pamoja na mikia sita ya tembo, kilo ishirini ya nyama ya nyati,ngozi moja ya paka pori na miiba ya Nungunungu.

Kamanda MWARUANDA, akizungumza  mbele ya Naibu Kamishna wa Polisi mstaafu VENANCE TOSSI ambaye ndiye anayeongoza kikosi kazi hicho, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kufanikisha kutokomeza ujangili.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment