Akizungumza na Balozi Luz ofisini Magogoni jijini Dar es Salaam
leo mchana (Jumatano, Aprili 29, 2015), Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo kwa
ushirikiano ambao ameutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi cha miaka
sita ambacho amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa nchini.
Balozi Luz ambaye amepangiwa kwenda Jordan kwenye kituo kipya,
alisema anaondoka nchini akiamini kwamba mtu atakayekuja kumpokea ataendelea
mambo aliyoyaanzisha ikiwemo mradi wa kufadhili utafiti na uendelezaji wa zao
la pamba kwenye kituo cha utafiti wa kilimo cha Ukiriguru, Mwanza.
Balozi Luz ambaye alifika kumuaga Waziri Mkuu, alitumia fursa hiyo
kumweleza Waziri Mkuu kwamba ubalozi huo umefanikiwa kupeleka Watanzania wawili
kusomea kozi za Uzamili (Masters’ Programme) kwenye vyuo vikuu vya Brazil.
“Wanafunzi hawa wawili waliondoka Februari mwaka huu, ni kati ya
wanafunzi saba waliofuzu lakini wengine watano walikosa ufadhili kutoka kwenye
taasisi zao. Mmoja anasomeaGeo-Physics na mwingine Oil
Engineering,” alisema Balozi Luz.
Balozi Luz ambaye anatarajia kuondoka nchini mapema mwezi ujao,
amepangiwa kituo kingine ambapo ataenda kuiwakilisha nchi yake nchini Jordan.
(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, APRILI 29, 2015.
Irene K. Bwire
0 comments:
Post a Comment