Watu 6 wauawa kufuatia shambulizi Kenya
Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi wengi ndani ya chuo hicho.
Inaelezwa kuwa wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa.
Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na magari ya ambalensi yamewasili katika eneo la tukio ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi.
Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.
Wanafunzi 27 wamefanikiwa kutoroka na sasa wako katika kituo kimoja cha kijeshi.
Kufikia sasa hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza shambulizi hilo ijapokuwa kundi la wapiganaji wa Somalia Al Shabaab limeshukiwa kutekeleza shambulizi hilo.
Chuo hicho ndio taasisi ya kipekee ya masomo ya juu katika eneo hilo kilichofunguliwa mwaka 2011 na kiko takriban kilomita 350 kutoka mji mkuu wa Nairobi.
0 comments:
Post a Comment