TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUZO YA JAMII ITAKAYOTOLEWA TAREHE 13 APRIL 2015
KATIKA UKUMBI WA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE, JIJINI DAR ES
SALAAM
MGENI RASMI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dokta Jakaya Mrisho Kikwete
WAGENI
WAALIKWA:
Mara
baada ya Hafla ya Tuzo ya Jamii ambapo Washindi wote watapewa Tuzo na Mgeni
Rasmi, Kutakuwa na Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii ambayo itahudhuriwa na
wageni wafuatao:
- Wapewa Tuzo,
- Familia za wapewa Tuzo,
- Viongozi Waandamizi wa Serikali,
- Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania,
- Viongozi wa vyama vya siasa na kijamii na Wafanyabiashara,
- Taasisi zisizo za kiserikali,
- Watu Mashuhuri na
- Wawakilishi kutoka makundi yenye mahitaji maalum ambapo kwa mwaka huu watawakilishwa na Watu wenye Ulemavu wa Ngozi-Albino
MUHIMU:
Tanzania Awards International
Ltd imepanga kufanya hafla ya utoaji wa Tuzo ya Jamii na kisha Dhifa ya Kitaifa
ya Tuzo ya Jamii siku ya tarehe 13 ya mwezi April ya kila mwaka kwa malengo ya
kuadhimisha Kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu
Julius Kambarege Nyerere.
Kuhusu Tanzania
Awards International Limited
Tanzania
Awards International Limited ni kampuni iliyosajiliwa kisheria nchini Tanzania
kwa Malengo ya Kufanya tafiti mbalimbali, Kutoa ushauri wa kisheria na kijamii,
kuandaa na kuratibu matukio pamoja na Uandaaji
na Utoaji wa Tuzo Ya Jamii.
Maana ya Tuzo ya Jamii
Tuzo ya Jamii ni Tuzo
inayotolewa kwa Taasisi na Watu binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zao katika
kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.
Malengo ya
Tuzo ya Jamii
- Kutambua, Kuthamini, Kuunga Mkono na Kutoa Tuzo kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.
- Kuikumbusha Jamii kuona umuhimu, kujali na Kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi au Mtu Binafsi katika kuleta Ustawi na Maendeleo ya Jamii
VIPENGELE
VYA TUZO YA JAMII 2015
Vipengele
vya Tuzo ya Jamii, hubadilika kila mwaka kulingana na aina na matokeo ya
Utafiti unaofanywa na Tanzania Awards International Limited. Kwa mwaka huu
(2015), Tuzo ya Jamii itakuwa na Vipengele Vikuu vinne (4) vifuatavyo:
- Tuzo ya Jamii 2015
- Tuzo ya jamii –Tuzo ya Heshima
- Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu
- Tuzo ya Jamii kwa Mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania
UFAFANUZI WA
KILA KIPENGELE CHA TUZO YA JAMII 2015
- Tuzo ya Jamii 2015
Tuzo hii
itatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na mchango na jitihada zake
katika kusaidia na kutetea Jamii.
Mshindi wa
Tuzo hii ya Jamii atapatikana kwa:
(a) Mhusika
mwenyewe kuwasilisha vielelezo au ushahidi wa mchango wake huo kwa Jamii
AU
(b) Kwa jamii
kupendekeza jina la mhusika kupitia mitandao ya kijamii
AU
(c) Kwa Kamati ya
Tuzo ya Jamii kufanya utafiti, kuchambua na kuteua jina moja miongoni mwa yale
yaliyopatikana kupitia kipengele (a) na (b)
Mshindi
wa Tuzo ya Jamii 2015 atatangazwa rasmi siku ya Hafla ya Tuzo ya Jamii
itakayofanyika tarehe 13 April 2015 katika Ukumbi wa Julius Nyerere
International Convention Centre, Jijini Dar es Salaam
2. Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima
Watakaopewa
Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima ni:
(a) Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na
(b) Hayati Nelson Mandela –Rais wa Kwanza Mzalendo
wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini
Tuzo hii ya Heshima kwa mwaka huu itatolewa kwa
Waasisi hao wawili kutokana na Jitihada na Mchango wao wa kipekee na uliotukuka
katika kutetea na Kulinda Maslahi ya Wanyonge
3.
Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu
Tuzo hii
inatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake
katika Kuelimisha, kulinda, kutetea na Kuimarisha Utawala Bora nchini Tanzania
Vigezo vinavyotumika kwa
mwaka huu katika kumpata mshindi wa Tuzo ya Jamii ya Haki za Bianadamu, ni hivi
vifuatavyo:
·
Weredi
wa Taasisi au Mtu Binafsi katika kufanya uchunguzi, Utafiti na kutoa taarifa
zake kwa uhuru, pasipo upendeleo wowote kwa Serikali, Chama, Kikundi au mtu Binafsi
·
Mchango
wa Mtu Binafsi au Taasisi katika Kuelimisha Jamii, kulinda, kutetea na kuhamasisha juu ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania.
·
Mchango
wa Mtu Binafsi au Taasisi katika kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha juu Amani,
utulivu, Usalama wa Raia na Mali zao na Utii wa Sheria kwa ujumla
- Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania
Mshindi wa Tuzo hii atatangazwa siku ya hafla ya
Tuzo ya Jamii baada ya mwanasiasa husika kupigiwa kura
nyingi kupitia mtandao wa Push mobile ambapo
mpigaji wa kura anatakiwa aende sehemu ya kuandika ujumbe mfupi wa maneno
katika simu yake ya Mkononi na kuandika namba ya Mwanasiasa husika, alafu
anatuma namba hiyo kwenda 15522.
Vigezo
vitakavyotumiwa na wapiga kura kupitia namba 15522 ni hivi vifuatavyo:
- Uadilifu, Uaminifu, Heshima na Utii kwa Jamii na sheria za nchi kwa Amani ya nchi yetu
- Jitihada binafsi katika kulinda na kutetea Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar, Umoja wa Kitaifa na Kijamii
- Uzoefu wa Uongozi wa Umma, Taasisi za Kimataifa na Mchango wake kwa Jamii.
- Matarajio, Mipango na nia ya Dhati ya Kuleta Maendeleo na Mafanikio kwa Watanzania
Orodha ya Wanasiasa wanaowania Tuzo ya Jamii
ya Mwanasiasa Kijana na Mtu Mzima Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania imepatikana
baada ya wanajamii kupendekeza mara nyingi jina la Mwanasiasa husika kupitia
Mtandao wa Push Mobile na mitandao mingine ya kijamii. Kamati ya Tuzo ya Jamii,
baada ya kupitia majina yote yaliyopendekezwa kupitia mbalimbali ikiwemo Push
Mobile, imepata orodha ifuatayo:
WATU WAZIMA
JINA LA MWANASIASA
|
NAMBA YA KUMPIGIA KURA
|
MHE.
MIZENGO PETER PINDA
|
MM01
|
MHE.
PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO
|
MM02
|
MHE.
DR. WILBROD PETER SLAA
|
MM03
|
MHE.
ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO
|
MM04
|
MHE.
SAMIA HASSAN SULUHU
|
MM05
|
MHE.
JAMES FRANCIS MBATIA
|
MM06
|
MHE.
DR. JOHN POMBE MAGUFULI
|
MM07
|
MHE.
DR. HARRISON GEORGE MWAKYEMBE
|
MM08
|
MHE.
PROF. IBRAHIM HARUNA LIPUMBA
|
MM09
|
MHE.
STEPHEN MASATU WASIRA
|
MM10
|
MHE.
BALOZI LIBERATA MULAMULA
|
MM11
|
MHE.
BENARD KAMILIUS MEMBE
|
MM12
|
MHE.
EDWARD NGOYAYI LOWASSA
|
MM13
|
VIJANA
JINA LA MWANASIASA
|
NAMBA YA KUMPIGIA KURA
|
MHE.
JANUARY YUSUPH MAKAMBA
|
MK01
|
MHE.
ZITTO ZUBERI KABWE
|
MK02
|
MHE.
MWIGULU LAMECK NCHEMBA
|
MK03
|
MHE.
HALIMA JAMES MDEE
|
MK04
|
MHE.
SAADA SALUM MKUYA
|
MK05
|
MHE.
LAZARO SAMUEL NYALANDU
|
MK06
|
MHE.
ESTHER AMOS BULAYA
|
MK07
|
MHE.
UMMY ALLY MWALIMU
|
MK08
|
MHE.
NAPE MOSES NNAUYE
|
MK09
|
MHE
.MBONI MHITA
|
MK10
|
MHE.
DAVID ZACHARIA KAFULILA
|
MK11
|
MHE.
VICKY PASCHAL KAMATA
|
MK12
|
MHE.
JOHN JOHN MNYIKA
|
MK13
|
Hatua
hii ya upigaji wa kura ni hatua ya mwisho katika mchakato wa kumpata mshindi wa
Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania (Kijana
na Mtu Mzima). Aidha, katika uamuzi wa Mshindi, matokeo ya upigaji wa kura
yatachukua asilimia Sabini (70%) na Asilimia Thelathini (30%) zitatumiwa na
Majaji ambao ni Kamati ya Tuzo ya Jamii 2015.
Zoezi la kumpigia kura Mwanasiasa Mwenye Mafanikio katika siasa za
Tanzania limeanza tarehe 10/03/2015 na litaendelea hadi tarehe 13/04/2015.
MCHAKATO WA JUMLA WA KUWAPATA WASHINDI NA KUWATANGAZA
Uendeshaji
wa Mchakato wa utoaji wa Tuzo ya Jamii huanzia kwenye Kitengo cha Utafiti,
Kumbukumbu na Majadiliano. Kitengo hiki, ndicho chenye jukumu la kufanya tafiti
mbalimbali kuhusiana na jambo husika.
- Kitengo cha Utafiti, Kumbukumbu na Majadiliano, kinapomaliza kazi yake ya Utafiti,huwasilisha mapendekezo yake kwenye Sekretarieti ya Kampuni ambayo inaundwa na wakuu wote wa vitengo vya kampuni pamoja Wajumbe wengine watatu ambao hufanya idadi yao kufikia saba (7). Kazi ya Sekretarieti ni kupitia taarifa kutoka kitengo cha ya Utafiti, kuichambua na kutoa mapendekezo yake na kuyawasilisha kwa Uongozi wa Kampuni.
- Taarifa ya Sekretariat huwasilishwa kwa uongozi wa Kampuni kwa ajili ya mapitio, mapendekezo au kwa uongozi kufanya mawasiliano na Vyanzo mbalimbali kabla ya uongozi wa kampuni kuiwasilisha taarifa hiyo kwenye Kamati nzima ya Tuzo ya Jamii
- Kamati ya Tuzo ya Jamii yenye Wajumbe ishirini na sita (26) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, hupitia, hujadili na kuchambua taarifa nzima inayohusiana na kipengele husika cha Tuzo ya Jamii.
- Kamati ya Tuzo ya Jamii baada ya kujiridhisha na uchambuzi iliyoufanya hupitisha, huthibitisha na kutangaza jina moja miongoni mwa yale yaliyohusishwa katika Utafiti husika. Maamuzi ya Kamati ya Tuzo ya Jamii huwa ni ya Mwisho.
- Mhusika aliyeshinda Tuzo ya Jamii katika kipengele husika hupewa taarifa rasmi Kuhusu ushindi wake
Imetolewa Machi 18,2015
Na Deonatus
Julius Malegesi
Mwenyekiti
Tanzania Awards International Ltd
0 comments:
Post a Comment