Image
Image

Gwajima atinga kituo cha polisi kishujaa kujibu tuhuma za kumtusi kiongozi wa kanisa katoliki nchini Polycarp Kardinal Pengo.


KIONGOZI wa kanisa la ufufuo na uzima askofu Joseph Gwajima amefika katika kituo kikuu cha polisi cha jijini Dar es salaam kwa ajili ya mahojiano na jeshi hilo kwa madai ya kutoa kauli,Matusi na maneno makali kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo,kama alivyo takiwa na jeshi la polisi kujisalimisha kituoni hapo.

Kuwasili kituoni hapo hivi leo Mchungaji Gwajima ni kutokana na wito wa jeshi la polisi kupitia vyombo vya habari kumtaka kiongozi huyo wa kanisa la ufufuo na uzima kufika kituon i hapo kwa mahojiano kwa madai ya kutoa maneno ya kashfa na matusi,kejeli  kwa kiongozi wa kanis katoliki nchini Polycarp Kardinal Pengo,ambapo kutokana na adha ya foleni kubwa ya magari katika jiji la Dar es salaam ilibidi kushuka katika gari lake na kutembea kwa miguu akiwa na walinzi wake kutoka katikati ya jiji hadi kituo kikuu cha polisi.

Baada ya  kuwasili katika kituoni hapo kwaajili ya mahojiano ya awali kutoka kwa vyombo vya habari ambapo askofu Gwajima yeye amesema maneno aliyoyatoa ni ya kumkemea kiongozi mwenzake wa kiroho kwa madai ya kukiuka msimamo wa viongozi wengine wa dini wa kuikataa mahakama ya kadhi.

Akijibu swali kuhusu sababu za kufanya hivyo badala ya kutumia maneno ya kistaarabu askofu gwajima amedai kuwa maneno aliyoyatoa ni maneno ya mungu huku akishangazwa na wito wa polisi kwa kuwa maneno hayo hakuyatoa kwa jeshi la polisi bali kwa kiongozi mwenzie w kiroho.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumezagaa picha za video zikiambatana na maneno ya kashfa kwenda kwa kiongozi wa kanisa katoliki nchini muadhama Polycarp Kardinal Pengo jambo lililofanya jeshi la polisi kumtaka kufika kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano zaidi.
Tazama Video ya Gwajima  anayotuhumiwa nayo kumtusi na kukejeli  Polycarp Kardinal Pengo.


TAARIFA YA AWALI KUTAKA GWAJIMA KUWASILI POLISI NDIO HII.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuripoti haraka Kituo Kikuu cha Polisi,  Dar es Salaam kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kashfa na matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Mapema wiki hii, mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp ilisambaza sauti ya Askofu Gwajima akitoa maneno makali ya kumkashfu Kardinali Pengo.
Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova kupitia taarifa yake kwa umma, alimtaka Askofu Gwajima kujisalimisha kituoni hapo na kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Kadhalika, taarifa hiyo ilieleza kuwa Kanda Maalumu ilipokea malalamiko ya kukashifiwa kwa Kardinali Pengo na jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hilo unaendelea.
“Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio, hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa kwenda kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam bila kukosa,” alisema Kamishna Kova.
“Ni muhimu sana kwa Askofu Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii,” aliongeza.
Machi 14, mwaka huu, Kardinali Pengo akizungumza katika ibada ya Kwaresima kwa Wanawake Wakatoliki Tanzania (Wawata), alitofautiana na Jukwaa la Wakristo linalojumuisha Baraza la Maaskofu Katoliki (Tec), kuhusu aina ya kura inayostahili kupigiwa Katiba Inayopendekezwa.
Wakati Jukwaa la Wakristo liliwataka waumini wake kuipigia Katiba Inayopendekezwa kura ya hapana, Kardinali Pengo alisema waisome na kuielewa na kupiga kura inayostahili kwa jinsi watakavyoona wao.
Kardinali Pengo alisema wao wakiwa viongozi wa watu, hawana mamlaka wala uwezo huo, bali wenye uwezo ni wananchi wenyewe.
Kauli ya Pengo ndiyo iliyoamsha hasira ya Gwajima na kutoa matamshi makali.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment