Mamia ya watu wakiwa wanashuhudia ndugu na jama zao wakizikwa katika kaburi moja ambalo kufuatia kupata ajali iliyohusiha basi la Nganga na fuso kisha
kuteketea kwa moto Iyovi ruaha wilayani kilosa katika
barabara ya Morogoro iringa.
Mamia ya wananchi wa kilosa na kilombero washiriki
katika mazishi ya pamoja kwa abiria waliokufa
kwenye ajali ya basi la Nganga.
Wakazi wa wilaya za kilosa na kilombero wamejitokeza kwa wingi katika kushuhudia maziko ya pamoja ya
watu kumi na tano kati ya kumi na tisa waliofariki katika ajali ya basi
ya Nganga ambalo liligongana na fuso kisha
kuwaka moto katika eneo la Iyovi na
kuzikwa katika kaburi la pamoja kwenye makaburi ya Msamvu ruaha wilayani kilosa
mkoani Morogoro.
Hili
ndilo kaburi moja ambalo wapendwa wetu
wanahifadhiwa humu ambapo greda lina wafukia baada ya kuingizwa wote humu ndani kwenye nyumba ya milele,kufuatia kupata ajali iliyohusiha basi la N ganga na fuso kasha
kuteketea kwa moto Iyovi ruaha wilayani kilosa katika
barabara ya Morogoro iringa.
Wakizungumza kwa niaba
ya serikali mkuu wa wilaya ya kilosa Bw John Henjewele amesema serikali
imewalazimu kufanya mazishi ya pamoja ya watu waliofariki kwenye ajali
hiyo ambao miili yao haijatambulika na kwamba serikali itaendelea na zoezi la
ukaguzi wa magari amkoani wa Morogoro ili kudhibiti ajali za mara
kwa mara na kupoteza maisha ya watu huku wengine wakiachwa na vilemalema vya
maisha ambapo mkuu wa wilaya ya kilombero Bw Lephy Gembe amewataka wananchi kuwa
na uvumilivu katika msiba mkubwa walioupata.
Hili
ndilo kaburi moja ambalo wapendwa wetu
wanahifadhiwa humu kufuatia kupata ajali iliyohusiha basi la N ganga na fuso kasha
kuteketea kwa moto Iyovi ruaha wilayani kilosa katika
barabara ya Morogoro iringa.
Kwa upande wake Diwani
wa kata ya ruaha Rahel Nyangasa amesema wamepokea msiba huo kwa
masikitiko makubwa kwani umekuwa ni pigo kubwa kwa wakazi wa wilaya hizo huku
ndugu na waombolezaji wakisema msiba huo siwakusahaulika kwani umewastua sana
ambapo naye muinjilisti wa kanisa la
kiinjili la kilutheri Issaya Chura akiomba serikali kuendelea kukabiliana na
madereva wabovu.
0 comments:
Post a Comment