Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif
Sharif Hamad,amefika katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, jijini dar es
salaam kufuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim
lipumba na wafuasi 29 wa chama hicho wanaotuhumiwa kutenda makosa
matatu,ikiwamo kufanya mkusanyiko na maandamano, kinyume cha sheria.
Maalim Seif, ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais
wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ amelakiwa na Prof. Lipumba na mamia wa
wafuasi wa chama hicho waliofika katika mahakama hiyo kufuatilia kesi hiyo
pamoja na kuwadhamini wafuasi wenzao.
Wakili wa upande wa jamhuri, amewasomea mashtaka
washtakiwa wawili kati ya 30, ambao ni Shhaweji Mketo na Hemed Abdallah, ambapo
wanakabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kufanya mkusanyiko usio halali na
maandamano, kinyume cha sheria.
Mashtaka mengine, wanayotuhumiwa nayo ni kula njama
kwa nia ya kutenda kosa na kufanya fujo, kinyume cha tamko la polisi
lililowazuia kukusanyika na kuandamana.
Wanatuhumiwa kutenda makosa hayo maeneo ya mbagala,
jijini dar es salaam ambapo wote walikana makosa hayo na wako nje kwa dhamana
hadi mei 6, mwaka huu kesi yao itakapokuja kwa ajili ya usikilizaji wa awali.
Watuhumiwa wengine 20 pia walipata dhamana baada ya
kukamilisha masharti ya dhamana na usikilizaji wa awali wa kesi yao utafanyika
mei 6, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama,
maalim Seif aliwashukuru wafuasi wa chama chake, kujitokeza kwa wingi na
waliowadhamini watuhumiwa akisema hiyo inaashiria kuwa tatizo linalowakabili
wenzao siyo lao peke yao, bali ni la wote.
0 comments:
Post a Comment