Image
Image

Wezi wa mifugo wauawa kwa kuchomwa moto Namtumbo Mkoani Ruvuma


Wezi wa mifugo wa kijiji cha Luegu wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wameuawa kwa kuchomwa moto baada ya wananchi wenye hasira kuwakamata usiku wa manane baada ya kuiba mbuzi kwa Amiri Mhuwa mkazi wa Kijiji cha Luegu.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jumamosi ambapo wezi hao walikurupushwa wakiiba mbuzi katika kijiji cha Nahoro na kisha kuelekea Kijiji cha Luegu na kuingia nyumbani mwa bwana Amiri Mhuwa na kuiba mbuzi wawili ambapo kelele za mbuzi hao zilimwamsha bwana Mhuwa na majirani wengine na kuanza kuwasaka wezi hao.
Hata hivyo wanachi wa Kijiji cha Nahoro licha ya kuwakurupusha wezi hao waliendelea kuwasaka. Kelele na mayowe ya wanachi kijiji cha Luegu ndizo zilizounganisha nguvu zao za kuwasaka wezi hao na kisha kuwakamata.
Baada ya wezi hao kukamwatwa walikatwakatwa na mapanga na kisha kuvirigiwa nyasi ambazo zilimwagiwa petroli na kisha kuwasha moto uliowaunguza na kuwaua kabisa wezi hao
Aidha Mtendaji wa kata ya Luegu Zainabu Enold Maduhu aliwataja waliouwawa kuwa ni Rajabu Tobhala Tango (31) na Abibu Moa (34) wote ni wakazi wa Kijiji cha Luegu, Mtwara Pachani.
Bi Maduhi aliongeza kuwa licha ya vijana hao kutuhumiwa kuwa ni vijana wanaoendesha tabia wizi katika kata hiyo aliwataka wananchi kufuata hatua za kisheria badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma bwana Mihayo Msikelah amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wananchi kuacha kuendelea kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa Marehemu waliouwawa walikutwa na kidhibitisho cha kuweza kuwatia hatiani kisheria.

Marehemu wote wawili walizikwa siku ya jumamosi kijijini hapo baada ya jeshi la polisi kutoa ruksa ya kuwazika marehemu
hao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment