Mkoani MBEYA baadhi ya watumiaji wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani wameilalamikia Halmashauri ya Jiji hilo kwa kuacha kukarabati jengo la abiria ambalo limechakaa na lina hatarisha maisha ya abiria.
Aidha imebainika pia kuwa kituo hicho kikuu cha mabasi kimekosa huduma za vyoo, na kuhatarisha afya za wasafiri na watu wanajishughulisha na kazi za kujiajiri kituoni hapo.
Akizungumzia changamoto hizo Mkuu wa wilaya ya Mbeya NYEREMBE MNASASABI amekiri kuwepo kwa changamoto ya kukosekana kwa huduma za choo kituoni hapo na kueleza kuwa ipo katika mpango wa muda mrefu wa serikali unaohusu kituo cha mabasi.
0 comments:
Post a Comment