Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa shughuli tayari kuzindua Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha
Programu ya Uongozi na Maadili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere
Kigamoni jijini Dar es salaam April 13, 2015, Kushoto kwake ni Waziri wa
Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa
Shadrack Mwakalila.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsimika rasmi Mzee
Pius Msekwa kuwa Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na
Maadili wakati wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika
Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza
Mzee Pius Msekwa akitoa shukurani baada ya kusimikwa rasmi kuwa
Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na Maadili wakati
wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya
Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake ni Waziri wa
Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack
Mwakalila.
0 comments:
Post a Comment