Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
CUF Profesa IBRAHIM HARUNA
LIPUMBA na wanachama we ngine 30 wa
chama hicho, leo wamefikishwa katika
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam waki shtakiwa kwa kosa la
kuandamana bila kufuata utaratibu .
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye
pia ni Katibu Mkuu wa - CUF -
maalim SEIF SHARIF HAMAD ni
miongoni mwa viongozi wanaohudhiria kesi
hiyo inayomkabili mwenyekiti wa chama hicho .
Profesa LIPUMBA na wafuasi 30 wa CUF wamefunguliwa mash i taka ya
kula njama, kukukusanyika na kuandamana bila ya kibali na kwa sasa wapo nje kwa dhamana .
Katika tukio la maandamano hayo , viongozi na wafuasi wa CUF
walipigwa na kukamatwa na polisi kwa madai ya kuandamana bila kibali wakati
wakiadhimisha mauaji ya wenzao waliouawa na polisi mwaka 2001.
Wafuasi hao walikuwa wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa
Rais wa Zanzibar mwaka 2000.
0 comments:
Post a Comment