Watu kumi wamefariki dunia na wengine zaidi ya arobaini wamejeruhiwa baada ya basi la UNIQUE lenye namba T148BKK na LORY la kampuni ya COCA COLA lenya namba za usajili T207BSA liliokua linakokota tela namba T655AJT katika kata ya Samuye mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi .
Amesema majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga
kwa matibabu na maiti wanahifadhiwa katika hospitali hiyo.
Kuhusu hali za madereva amesema hali ya dereva wa basi ni mbaya
isipokuwa dereva wa lori ambaye amekimbia baada ya ajali, amejisalimisha polisi
0 comments:
Post a Comment