Afisa wa mawasiliano wa Safa Dominic Chimhavi
amewataka wote wenye ushahidi dhidi ya shirikisho hilo kuuweka wazi ilikuondoa
shaka iliyoibuka kufuatia kukamatwa kwa maafisa wakuu wa FIFA.
Tuhuma hizo ziliibuka baada ya polisi wa Uswisi
kuwakamata maafisa wakuu wanaotuhumiwa kwa kushiriki ufisadi na kula kiinua
mgongo cha takriban dola million 150 ndani ya kipindi cha miaka 20.
Tuhuma hizo zilifuatia uchunguzi wa idara ya ujasusi
ya Marekani.
Kwa Upande wake, waziri wa michezo wa Afrika Kusini
amekanusha kuwa shirikisho la soka nchini humo lilitoa hongo ya dola milioni 10
ili taifa hilo lipewe uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2010.
Waziri Fikile Mbalula alisema kuwa ni uongo mtupu na
kuwa serikali haikumlipa yeyote.
Uchunguzi wa vitendo vya rushwa ndani ya Fifa
umebainisha kuwa viongozi 3 walipokea hongo ya dola milioni kumi iliwanachama
watatu waipigie kura Afrika Kusini kuandaa kombe la dunia la 2010.
Hata madai hayo yanafuatia mawasiliano baina ya SAFA
na wanakamati wengine wa FIFA ambapo serikali iliahidi kutoa dola milioni 10
iwapo makamu wa rais wakati huo Jack Warner angewashawishi wanawkamati wenza
kuipigia kura Afrika kusini badala ya Morocco.
Kulingana na taarifa ya upande wa mashtaka Afrika
kusini ilishindwa kulipa pesa hizo moja kwa moja na hivyo ikapanga FIFA iwalipe
moja kwa moja Ripoti hiyo ya FBI ilisema.
Awali waziri wa ofisi ya rais Jeff Radebe alikanusha
madai ya kutolewa kwa hongo yeyote akisema kuwa kamati andalazi iliwajibikia
kila senti iliyopata kwaajili ya maandalizi ya kombe la dunia lililofanyika
mwaka wa 2010 kwa mara ya kwanza ndani ya bara la Afrika.
Serikali ya Uswiss imesema itaidhinisha haraka
kusafirishwa kwa maafisa hao waliokamatwa kwenda Marekani .
Mwanzoni mwa mwezi huu, Blatter alisema anafahamu
baadhi ya wafanyakazi wenzake wa zamani walikuwa wakichunguzwa lakini
amekanusha kuwa uchunguzi huo ulimhusu pia.
0 comments:
Post a Comment