Hata hivyo rais wa Urusi
Vladimir Putin amemuunga mkono bwana Blatter akisema bila shaka hizo ni njama
za Marekani za kumtaka Blatter asiwanie tena uongozi wa FIFA.
Wakati huohuo Mmoja ya
wafadhili wakuu wa kombe la dunia anasema kuwa huenda akalazimika kutathmini
upya ufadhili wake kwa FIFA ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kurejesha
hadhi ya mchezo wa kandanda.
Taarifa kutoka kwa kampuni ya
VISA inatolewa kufuatia visa vya kukamatwa kwa maafisa 7 wa vyeo vya juu wa
FIFA kwa madai ya ulaji rushwa.
Wafadhili wengine nao wametoa
maoni yao.
Kampuni ya Coca-Cola ilisema
kuwa madai hayo yamechafua hadhi ya kombe la dunia huku kampuni ya magari ya
Hyundai ikisema ina wasiwasi wa kesi zinazowaandama maafisa wa FIFA.
Blatter anawania muhula wake wa tano kama rais wa FIFA
katika uchaguzi ulioratibiwa kufanyika hapo kesho
0 comments:
Post a Comment