Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemtaka kiungo wao, Ramadhani Singano
‘Messi’ apeleke kopi ya mkataba ili kumaliza ubishi.
Singano amekuwa akilalamika
kwamba Simba wamecheza mchezo na kumuongezea mwaka mmoja kwenye mkataba wake
ulio TFF.
Lakini Hans Poppe amesisitiza
mkataba wa Messi unamalizika mwakani na si mwaka huu kama ambavyo amekuwa
akisema kiungo huyo.
“Yeye alete mkataba tu,
kawaida kunakuwa na kopi tatu. Yake, yetu na ya TFF. Sasa alete yake, sisi
tutoe ili kuangalia wapi kuna tatizo.
“Nafikiri haitakuwa busara
hili suala kuendelea kukuzwa wakati kulimaliza ni lahisi na mikataba yote ipo,”
alisema Hans Poppe.
Hata hivyo, Hans Poppe alisisitiza kwamba anachotakiwa Messi ni kuwasilisha mkataba orijino na si kopi.
"Kopi mtu anaweza kuichezea, hivyo hatutakubali. Alete ule orijino kama ambavyo sisi tutafanya," alisema.

0 comments:
Post a Comment