Akitoa taarifa ya mradi wa
ujenzi wa choo hicho na kukabidhi msaada wa viti 30 na magodoro 60 kwa ajili ya
malazi ya wazee hao vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 mratibu wa EASY
FLEX Bi. Happyness Kihama amesema taasisi yake imeamua kuwajengea choo na kutoa
msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo yanayowakabili wazee hao kituoni
hapo ikiwa pia ni kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia
hovyo.
Akipokea msaada huo na jengo
la choo chenye matundu manne kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw. Ally Rufunga
mstahiki meya wa manispaa ya shinyanga Bw. Gullam Hafidh pamoja na kuishukuru
taasisi hiyo ameitaka jamii ya watanzania kuwa na mwamko wa kuanza kuwasaidia
wazee na watu wenye mahitaji maalum badala ya kusubiri misaada kutoka kwa
wahisani wa nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikidhalilisha utu wa mtanzania.
Kwa upande wao mlezi msaidizi
wa kituo hicho Bi. Evodia Ndaka na mwenyekiti wa makazi hayo simon maganga wameiomba
serikali kuzifanyia ukarabati mkubwa nyumba za makazi hayo ya wazee kutokana na
majengo yake kuchakaa hali inayowafanya waishi kwa wasiwasi mkubwa na kwamba
wamekuwa wakilazimika kuzihama wakati wa mvua inaponyesha kutokana
na kuvuja huku nyingi kati ya hizo tayari sehemu za kuta zake zimebomoka.
0 comments:
Post a Comment