Jaji alibaini kuwa mmoja wa
wahudumu wa hospitali ya Aghakhan alizembea katika kupachika mwilini dawa ya
kuzuia utungwaji wa mimba iliyochaguliwa na mwanamke kwenye mkono wake, licha
ya kwamba mwanamke huyo alifanyiwa upasuaji mdogo kwa ajili ya kuzuia uzazi.
Mwandishi wetu Anne Soy anarifu zaidi kuhusu uamuzi huo wa mahakama usio wa
kawaida.
Muathirika aliimbia mahakama
kuwa yeye na mumewe walikuwa tayari na watoto wawili na kwamba hawakutaka
kupata mtoto mwingine . Kwa hiyo kutokana na ushauri wa hospitali mama huyo
alipachikiwa dawa ya kuzuia uzazi ambayo ingelimzuia kupata ujauzito kwa miaka
mitatu . Lakini mwaka mmoja baadae aligundua kuwa alikuwa mjamzito .
Ameiambia mahakama kwamba
mimba ambayo hakuipanga ilimsababishia maumivu ya mfadhaiko mkubwa , msongo wa
mawazo , matatizo ya kifedha na matatizo ya unyumba. Jaji alisema kuwa
mshitakiwa ambae ni Hospitali ya Aga Khan , iliwasilisha nyaraka , lakini
haikuwepo mahakamani wakati wa kesi hiyo .
Kesi iliendelea na hatimae
jaji aliamua kuwa mhudumu wa hospitali alizembea kazini . Aliamuru mama
aliyeshitaki hospitali ya Agakhan alipwe fidia ya dola elfu tano kwa hasara
iliyosababishwa na apewe malipo ya dola elfu 43,000 za gharama ya maisha mtoto
tangu kuzaliwa hadi atakapotimiza miaka 18.
0 comments:
Post a Comment