Katika taarifa iliyotolewa na rais wa Baraza hilo,
Raimonda MurmokaitÄ—, wanachama wa Baraza la Usalama wametuma rambirambi zao kwa
familia za wahanga wa shambulizi hilo na kwa serikali ya Saudia.
Wajumbe hao wamekariri tena kuwa ISIL ni lazima
ishindwe, na kwamba msimamo mkali, ukatili na chuki linaloeneza kundi hilo, ni
lazima vikomeshwe. Wamesema vitendo kama hivyo vya kinyama haviwatishi, bali
vinaimarisha ari yao kwamba kunapaswa kuwepo juhudi za pamoja miongoni mwa
serikali na taasisi, zikiwemo zile za kikanda, ili kupambana na ISIL na makundi
yanayoiunga mkono kama Ansar Al Shari'a.
Aidha, wajumbe hao wa Baraza la Usalama wamelaani
vikali vitendo vya kinyama vinavyotekelezwa na ISIL nchini Syria, vikiwemo
kuuteka mji wa Palmyra kwa njia ya kikatili.
Wameelezea wasiwasi wao kuhusu maelfu ya wakazi wa
mji huo wa Palmyra, na kuhusu wote waliolazimika kuhama kutokana na vitendo vya
ISIL.


0 comments:
Post a Comment