Onyo hilo limetolewa wilayani Rungwe na
mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo, Chadema, Freeman Mbowe wakati
akizungumza na viongozi wa ngazi ya wilaya, majimbo na watu ambao wametangaza
nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chadema .
Katika hatua nyingine mbowe amesema kuwa chama chake
kinapambana kushika dola sio kwa lengo la kwenda ikulu kulipiza kisasi,bali
kinataka kushika madaraka ili kuwaletea watanzania neema ya maendeleo kwa
kufanya mambo ambayo chama cha mapinduzi kimeshindwa kuwafanyia watanzania.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chadema mkoa wa mbeya,
joseph mwachembe, maarufu kwa jina la china amelalamikia tume ya taifa ya
uchaguzi, NEC, kwa kutowashirikisha wadau ipasavyo katika zoezi la uandikishaji
wapigakura kwenye Daftari la kudumu kwa Teknolojia ya Biometric Voters Registration,
BVR.




0 comments:
Post a Comment