Na Mwandishi Maalum, New York
Wakati hali ya kisiasa na kiusalama ikiendelea
kuwa ya sintofahamu Nchini Burundi, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon, ameelezea kutiwa moyo na juhudi mbambali
zinazolenga kurejesha hali ya amani na usalama nchi humo.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu,
siku ya Ijumaa hapa Umoja wa Mataifa, imesema, katibu Mkuu
anatiwa moyo na juhudi zinazofanywa na makundi mbalimbali ya
kikanda, ya kidini, ya kijamii, vyama vya siasa pamoja na Mwakilishi
Wake Maalum katika Eneo la Maziwa Makuu katika kuhakikisha
kwamba mgogoro na sitofahamu iliyoikumba Burundi inatafutiwa ufumbuzi.
Wahusika wakuu ambao Ban Ki Moon ameelezea kutiwa
moyo na juhudi zao za kuleta amani nchini Burundi ni pamoja na Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo ipo chini ya
uenyekiti wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Umoja
wa Afrika ( AU), Soko la pamoja la Afrika Mashariki na
Kusini mwa Afrika ( COMESA),
Mkutano wa Kimataifa wa Eneo la Maziwa Makuu (
ICGLR) na Mwakilishi wake Maalum katika eneo la maziwa Makuu
Bw. Said Djinnit.
“ Katibu Mkuu anawapongea washirika wote
wanaoshiriki mchakato huo pamoja na mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa, hususani
katika kupunguza hali ya wasiwasi na sintofahamu na kujenga
mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi huru, wa haki, jumuishi na wa
amani.” Inasomeka Taarifa ya katibu Mkuu
Hata hiyo pamoja na kutiwa moyo na kazi
nzuri inayoendelea kufanyika, Katibu Mkuu ameelezea wasi wasi wake
hali mbaya ya kibinadamu inayowakabiri wakimbizi kutoka Burundi
ambao wamekimbilia nchi za jirani ikiwamo Tanzania.
Pamoja na wasiwasi huo Ban Ki Moon
amezipongeza nchi jirani kwa kutoa misaada ya kibinadamu ikiwa ni
pamoja na kuwahifadhi wakimbizi hao. Huku akitoa wito kwa Serikali
ya Burundi kuandaa mazingira ya kuwarejesha nchi humo raia wake
waliokimbia machafuko.
Vile vile Katibu Mkuuu, amewahimiza wadau mbalimbali
kuendelea na majadiliano kwa lengo la kufikia makubaliano ya jumla
katika maeneo yote ambayo wameyaainisha. Huku akithibitisha utayari
wa Umoja wa Mataifa katika kuwasaidia wananchi wa Burundi
na Kanda kwa ujumla katika mchakato huu.
TaarifakutokaMashirikayaKimataifalikiwamola
wakimbizi, UNHCR zinazonyeshakwambatangumweziAprilimwakahuu, jumlayawananchi
100,000 wa Burundi wakimbianchiyaonakuvukamipakanakuingiakatikanchiza Tanzania,
Rwanda naJamhuriyaKidemokrasiayaKongo.
Wimbihilo la wakimbizi,
limesababishakuibukakwaugonjwawakipindupindukatikakambiiliyokoKigomaugonjwaambaoumesabishavifovyawatu
37 kwamujibuwa UNHCR nakwambaSerikaliya Tanzania imekwisha kutangaza uwepo
wa ugonjwa huo.


0 comments:
Post a Comment