Wakati serikali ya Piere Nkuruziza ikielezwa
kupinduliwa na jeshi la nchi hiyo,Rais huyo yupo hapa nchini Tanzania katika
kikao cha Marais wa Jumuiya wa Afrika Mashariki, EAC jijini Dar es Salaam katika
kikao cha dharura.
Katika kikao hicho Marais wa Tanzania, Kenya, Uganda,Rwanda
na Burundi watajadili hali ya sintofahamu inayoendelea nchini Burundi. Kikao hicho
kimeitishwa na Mwenyekiti wa sasa wa EAC,Rais Jakaya Kikwete, kwa lengo la
kujadili vurugu ambazo zimekuwa zikitawala nchini Burundi.
Hata hivyo wananchi nchini Burundi wanapinga suala
la Rais huyo kutaka kujiongezea muongo mwingine wa kuingoza nchi hiyo ikiwa
tayari amesha kwisha kaa miongo miwili madarakani,Mahakama nchini humo pia
ilimpatia kibali cha kuendelea kutangaza nia ya kugombea nchini Burundi na
kuiongoza nchi hiyo.
Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Meja Jenerali Godefroid Bniyombareh ametoa taarifa kupitia kituo cha Radio cha Isanganiro akisema
serikali ya Nkurunziza imevunjwa.
Askari wamezingira kituo cha utangazaji cha serikali
nchini Burudi baada ya afisa wa jeshi kutangaza kuipindua serikali ya Rais ya
Piere Nkurunziza wa Burundi.
0 comments:
Post a Comment