Sheria hii ya kirais inatoa ongezeko la nakisi na
inapanga kupunguza bajeti za baadhi ya wizara kwa minajili ya kupatikana kwa
euro milioni 25 sawa na bilioni 44 sarafu ya Burundi.
"
Kutokana na uharaka na umuhimu wa kuiwezesha Tume Huru ya kitaifa ya Uchaguzi
kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi ...", hayo ni maneno ambayo tunaweza
kusoma kwenye sheria ya kirais yenye nambari 100/160, ya tarehe 21 Mei mwaka
2015, ambayo RFI imepata nakala. Sheria hiyo imetiliwa saini na rais Pierre
Nkurunziza, makamu wake wa pili na Waziri wa Fedha.
Rais wa Burundi ameamuru shughuli mbalimbali ili
pesa bilioni 44 sarafu ya Burundi ziweze kupatikana na hivyo kufadhili uchaguzi
huo. Ili kupata kiwango hiki, kulingana na waraka huo, deni la ndani lazima
" liwekwe kando ". Deni hili linakadiriwa kuwa sawa na bilioni 28
sarafu ya Burundi. Bilioni moja inatazamiwa kupatikana kupitia utaratibu mpya
uliyowekwa ambao unajulikana kwa jina la " bidhaa nyingine " na
bilioni 15 zitaondolewa kwenye taasisi nyingine. Miongoni mwa taasisi ambazo
bajeti zao zitapunguzwa ni ofisi ya rais katika mradi wake unaojulikana kama
"msaada kwa jitihada nzuri".
Si chini ya wizara tisa ambazo zitaathirika, ikiwa
ni pamoja na wizara ya mambo ya Ndani, Sheria, Afya, Kilimo na wizara ya Elimu.
Upande wa wanadiplomasia kutoka nchi za Magharibi,
hali hiyo inatia wasiwasi.
"
Shirika la fedha dunia IMF na Benki ya Dunia vinaweza kujiondoa nchini Burundi
kutokana na ongezeko la nakisi", amesema mmoja kati ya wanadiplomasia
kutoka nchi za Magharibi, kabla ya kuongeza " viongozi wa Burundi wanataka
uchaguzi ufanyike kwa hali na mali, bila kuzingatia athari ambazo zaweza
kujitokeza baadae ".
"
Afadhali kuwepo na mdororo wa kibajeti badala ya mgogoro wa kisiasa na usalama
unaotokana na kutokuwepo na taasisi za uongozi wa nchi ", amejibu Willy
Nyamitwe, mshauri mkuu wa rais Nkurunziza anayehusika na masuala ya
mawasiliano.
"Ananaongeza
ubaya juu ya ubaya"
"
Nadhani ni kutoelewa majukumu yake, kwa rais anayemaliza muda wake na ambaye
anasaini sheria ihusuyo bajeti ambayo inakakabiliwa na upungufu. Atachukua
fedha kutoka wizara mbalimbali wakati ambapo wizara hizo hizo hazina pesa za
kutosha na huenda wafanyakazi wakaanza mgomo", Jean Minani, kiongozi wa
chama cha upinzani cha FRODEBU Nyakuri.


0 comments:
Post a Comment