Dr. Bilal ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati
akifungua mkutano wa tano wa wakuu wataasisi za kupambana na rushwa kwa nchi 54
wanachama wa jumuiya ya madola ambapo amebainisha kuwa bila usafi wa viongozi
wa kisiasa na watumishi wa umma katika kukataa
Rushwa tatizo la hilo bado litaendelea kuwa
changamoto katika kufikia malengo ya maendeleo.
Jumuiya ya afrika mashariki ikitanguliwa na rwanda
waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora Kapteni mstaafu George Mkuchika
amekiri kuwa tatizo la rushwa hasa kwa viongozi wa nafasi za juu serikali
inatia doa utawala bora nchini na kusema kuwa mapambano hayo hasa kwa watumishi
wa umma yanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukuwaji wa technologia.
Kwa upande wake mkurugenzi wa tasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa nchini takukuru Dr. Edward Hosea amesema kuwa miongoni mwa
maeneo sugu ya utoaji na upokeaji rushwa ni katika kipindi cha uchaguzi na hapa
anaeleza jinsi Takukuru ilivyojiandaa kupambana na rushwa katika uchaguzi mkuu
wa mwezi October mwaka huu.


0 comments:
Post a Comment