Serikali imetakiwa kuhakisha kuwa
inaongeza nguvu katika kuhakisha kuwa
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanakomeshwa kwani
tatizo hilo limekuwepo kwa muda mrefu
lakini ufumbuzi wake umebaki kuwa
kitendawili na hivyo kuwa ni aibu na
fedheha kubwa kwa taifa.
Hayo yamesemwa katika hotuba
ya msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni
wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Mh.
Salum Khalfan Barwany
iliyosomwa na Mh. Esther matiku ambapo amesema sasa
suala la mauji ya alibino limekuwa tishio
kubwa.
Kwa upande wa kamati ya kudumu
ya maaendeleo ya jamii imesema kuwa sababu
kubwa ya mambo mengi kushindwa kwenda kama
inavyotakiwa ni serikli kutenga fedha katika wizara
zake hasa ya maendeleo ya jamii na
kutokuzikupeleka na hata ikipeleka haipeleki kwa wakati.
Awali katika kikao hicho Mh.Sophia Simba waziri wa wizara ya maendeleo ya jamii
jinsi na watoto na Mh. Gaudentia Kabaka waziri wa kazi na
ajira waliwasilisha bajetia za wizara zao ambapo kila mtu
alijinadi ni kwa namna gani atakavyotumia fedha hizo.
Wakichangia bajeti hizo baadhi ya wabunge
wamesema bado tatizo la ajira ni kubwa nchini ukilinganisha na
ahadi zinazotolewa za ajira na baadhi yao wakitaka vyuo
vya maendeleo ya jamii vitumike ipasavyo ili kusaidia
kupatikana kwa wataalamu.


0 comments:
Post a Comment