Akimkaribisha mgeni rasmi kaimu mkuu wa wilaya ya Mbongwe
ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya bukombe amani mwenegoha amewataka wananchi
kuacha kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kupata tiba ya Fistula na badala yake
wawapeleke hospitali ili kupatiwa tiba sahihi.
Naye msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto amesema iko
dhana potofu ya kuwa mwanamke anayeugua fistula alikuwa na wanaume wengi
kipindi cha ujauzito jambo ambalo si kweli hata kidogo.
Awali akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya
kutokomeza ugonjwa wa fistula kwa akina mama waliopata uzazi pingamizi Naibu
waziri tamisemi katika ofisi ya waziri mkuu Kassimu Majaliwa amesema vita ya
kupambana na ugonjwa wa fistula ni ya kila mtu hivyo kuwataka wananchi kutoa
ushirikiano pale watakapomuona mgonjwa.
Kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Fistula inafanywa
na mashirika yasiyo ya kiserikali kama hospitali ya CCBRT,VODACOMFOUNDATION,UNFP,AMREF
ambapo mikoa mitano itatembelewa na kupata elimu hiyo kwa awamu ya kwanza.


0 comments:
Post a Comment