Chama tawala cha Ethiopia kinaelekea kushinda kwa
kishindo uchaguzi mkuu wa nchi hiyo huku wapinzani wakilalamika kwa kudai
kwamba wakati wa zoezi la kupiga kura wafuasi wao walinyanyaswa.
Uchaguzi huo ni wa kwanza tangu mwaka 2012 alipofariki
waziri mkuu wa nchi hiyo Bwana Melesi Zenawi na kurithiwa na Bwana Hailemarian
Desalegn.
Akizungumza baada ya kupiga kura kwenye jimbo lake
la Gununo kilomita 330 magharibi ya mji mkuu wa nchi hiyo, Addis Ababa bwana Desalegn
alisema hakukuwa na ukandamizaji wowote katika uchaguzi huo.




0 comments:
Post a Comment