Image
Image

Kampuni ya simu za mkononi TIGO yatoa madawati yenye tahamani ya shilingi milioni mia moja.


Kampuni ya simu za mikononi (TIGO) kanda ya ziwa imetoa msaada wa madawati mia sita yenye thamani ya shilingi milioni mia moja za kitanzania  kwa shule za msingi nane za mkoa wa shinyanga kwaajili ya  kupunguza uhaba wa madawati unaozikumba shule nyingi mkoani humo.
Msaada huo wa madawati umeelezwa kuwa utasaidia kuimarisha kiwango cha elimu na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati hayo mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Bw.Ally Maswanya amesema kampuni yake inatambua umuhimu wa elimu kwa watanzania na kampuni imeamua kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii katika upande wa elimu ili kuendelea kuimarisha sekta hiyo.
Hata hivyo naye aimu katibu tawala wa mkoa wa shinyanga Bw.Projectus Rubwanzibwa amesema msaada huo utasaidia kupunguza tatizo sugu la madawati linaoukabili mkoa wa shinyanga kwa muda mrefu na kukuza kiwango cha elimu huku baadhi ya wanafunzi wa shule zilizopata mzaada huo wakionyesha furaha waliyoipata na kwa upande mwingine wakiahidi kufanya vizuri katika masomo yao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment