Image
Image

Msemaji wa jeshi la Burundi akanusha habari kuhusu mgawanyiko ndani ya jeshi.


Msemaji wa jeshi la Burundi Kanali Gaspard Baratuza amekanusha habari kuhusu kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya jeshi la Burundi na habari kuwa waziri mpya wa ulinzi wa nchi hiyo Emmanuel Ntahomvukiye alizuiwa kuingia ofisini mwake. Amesema habari hizo ni uvumi na hajui aliyeeneza uvumi huo ana nia gani.
Wakati huohuo, rais Pierre Nkurunziza amesaini amri ya kuitisha mkutano maalumu wa mabaraza mawili ya bunge la nchi hiyo Mei 20 na 21, bila kueleza sababu ya kuitisha mkutano huo.

Habari nyingine zinasema Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeihimiza jumuiya ya kimataifa kutoa msaada kutokana na idadi ya wakimbizi kutoka Burundi walioambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kuongezeka hadi kufikia zaidi ya 1,000.

Mjumbe maalumu wa shirika hilo nchini Tanzania Joyce Mends-Cole amesema hali ni mbaya. Mpaka sasa wakimbizi 17 wa Burundi wamefariki kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment