Image
Image

News Alert:Mwigulu Nchemba avunja ukimya Bungeni juu ya madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu yaliyosababisha wagome.




Serikali imewaomba radhi wanafunzi wa vyuo vikuu kwa hatua walizopitia kutokana na fedha za kujikimu kuchelewa na kwamba fedha zimeshatoka hazina huku ikizitaka taasisi zinakopita fedha hizo kuhakikisha zinawafikia wanafunzi leo leo.
Naibu waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba amelazimika kutoa ufafanuzi huo juu ya madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu yaliyosababisha  jana wagome, baada ya Mh .Esther  Bulaya mbunge wa viti maalum kuomba muongozo wa mwenyekiti kuhusiana na suala hilo Bungeni mjini Dodoma.

Kauli hiyo imrtolewa baada ya jana wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani waligoma kuingia darasani kwa madai ya kutopewa fedha za kujikimu kwa zaidi ya wiki 11 huku wakitaja gharama za maisha zikiwa zimepanda mara dufu.

Katika viwanja vya chuo kikuu jijini Dar es Salaam walisema endapo serikali haitasikia kilio chao na kukipatia ufumbuzi basi wataendelea na mgomo hadi fedha zitakpoingia kwenye akaunti zao. 

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandara pamoja na kukiri madai ya wanafunzi elfu saba kati ya zaidi ya elfu kumi wanaofadhiliwa na serikali kupitia bodi ya mikopo kucheleweshewa fedha zao kuwa ya msingi amesema tayari amezungumza na bodi ya mikopo ambao wamemwahidi kuleta fedha zao haraka iwezekanavyo na kuwaomba wanafunzi kurejea madarasani kuendelea na masomo.

Wakati huohuo takribani wanafunzi 400 wa chuo kikuu cha Mt. Josephu cha Mbezi jijini Dar es Salaam mwaka wa kwanza wamesimamishwa masomo kwa muda usiojulikana baada ya kugoma kuingia madarasani wakidai fedha za kujikim kutoka bodi ya mikopo tangu mwezi Desemba mwaka jana hadi sasa wakieleza kuishindwa kuendesha maisha yao ya shule na kuhimili mazingira ya kupangha nyumba mitaani.

Katika taarifa ya kusimamisha wanafunzi hao iliyotolewa na makamu mkuu wa chuo cha Mt.Josephu Bw.Loyola Proteep aliyeambatana na mkuu wa wanafunzi maarufu kama Dean anakiri madai ya wanafunzi hao kuwa ya msingi na kuongeza kuwa waliwaomba utulivu na kuingia Madarasani wakati wakifuatilia madai yao bodi ya mikopo bila ya mafanikio na uongozi kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza hadi vikao vya bodi vitakapoamua vinginevyo.
     Kauli ya Mwigulu Nchemba Bungeni leo ndiyo hii.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment