Promosheni hii imeanzishwa kutokana na kuonenakana kuwepo kwa mahitaji makubwa
ya matumizi ya data katika kupata taarifa kupitia mtandao wa
intaneti.Vodacom Tanzania siku zote imekuwa mstari wa mbele kubuni huduma
zinazoendana na matakwa ya wateja wake na kuwarahisishia maisha katika nyanja
ya elimu,afya,Kilimo,burudani,huduma za kibenki na huduma nyinginezo za
kurahisisha biashara mbalimbali.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii leo,Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa
Kampuni hiyo Kelvin Twissa amesema “Kupitia promosheni hii ya ”Good Morning
Tanzania” Vodacom tutawaunganisha wateja wetu na sehemu nyingine za dunia bure
kila siku.Ofa hii inawawezesha wateja wetu kufanya shughuli zao mapema
bure kupitia mtandao wa intaneti ikiwemo kuwasiliana na marafiki,kupata habari
mbalimbali za kitaifa na kimataifa na matumizi mengineyo mengi yanayoweza
kufanyika kupitia kwenye mtandao wa internet.
Promosheni ya ”Good Morning Tanzania”imeadaliwa mahususi kukidhi matakwa ya
wateja wa Vodacom ili kuwarahisishia maisha na watanzania wametakiwa kujiunga
na familia ya Vodacom waweze kutumia fursa hii kupata wakipendacho
kupitia teknolojia ya simu za mkononi.
Ili kupata huduma hii mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga namba *149*01#
ambapo atapata maelekezo zaidi na kuanza kupakua na kuperuzi intaneti na kuweza
kupata kwa urahisi anachohitaji akiwa ametulia nyumbani kwake.


0 comments:
Post a Comment