Mashirika ya misaada ya kimataifa yamesema kuwa yameondoa wafanyakazi wao walioko jimbo la Unity State kaskazini mwa Sudan Kusini wakilalamikia kuongezeka kwa mapigano.
Mashirika ya misaada ya kimataifa yamesema kuwa yameondoa wafanyakazi wao walioko jimbo la Unity State kaskazini mwa Sudan Kusini wakilalamikia kuongezeka kwa mapigano kati ya waasi na jeshi la serikali. Shirika la msalaba mwekundu la lile la Medicine Sans Frontier (MSF) ni baadhi ya yale yalioondoa wafanyakazi wao.
Kiongozi wa MSF nchini humo Paul Critchley amesema kuondoka kwao kunasikitisha kwani raia wanaoathiriwa na vita watabaki bila huduma za afya huku chama cha mslaba mwekundu kikielezea masikitiko yake kuhusu raia wanaokimbia makwao kutokanna na vita.
Kulingana na Umoja wa Mataifa karibu watu 100, 000 wamefurushwa makwao wiki jana wakati vita vilipozuka upya.
0 comments:
Post a Comment