Beki huyo aliyesajiliwa
kutoka JKT Ruvu, alisema kuwa amefurahi mno kumwaga wino Msimbazi juzi Jumatano
usiku, lakini kubwa ambalo amepania kulifanya kwa kikosi hicho ni kuhakikisha
inakata minyororo ya utumwa ya kushindwa kutwaa taji la Ligi Kuu Bara tangu
msimu wa 2011/2012.
Faki ambaye jana Alhamisi
mchana alirejea kwao Zanzibar kwa ajili ya mapumziko alisema: “Ninafuraha ya
kuwa ndani ya Simba na nina malengo ya kuipa ubingwa msimu ujao.
“Nitahakikisha ninacheza kwa
kujitoa na kupambana kuipa Simba heshima ya kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo
wowote.
“Lakini pia ninajua kuwa
Simba wana upinzani mkubwa na Yanga, hivyo ninajua heshima kubwa ya mchezaji
kwenye hizo klabu huchangiwa na mchezo wa watani, hivyo nitahakikisha
ninaendeleza rekodi bora walizonazo Simba kwa sasa za kuifunga Yanga muda
wowote ule.
“Yanga kwa Simba si kitu,
mimi nimekuja Simba kufanya kazi na moja ya kazi zangu Simba itakuwa ni
kuwadhibiti Yanga, lakini pia timu zote zitakazocheza dhidi yetu.”
Faki ambaye anasifika kwa
nguvu na akili ya uwanjani, aliongeza kuwa msimu uliopita akiwa JKT Ruvu
alipata nafasi ya kucheza dhidi ya Yanga na kudai kuwa ni timu ya kawaida licha
ya kwamba waliwafunga katika mechi zote mbili.
“Ninachokiona kwa Yanga ni
uzoefu tu, lakini ni timu ya kawaida na kutua kwangu Msimbazi nikiwa na wakali
wengine, nina hakika Yanga watataabika sana msimu ujao,” alitamba Faki.
Mbali ya mchezaji
huyo, pia kiraka za zamani wa Azam, Samir Nuhu alisaini mkataba na Simba
juzi usiku jijini Dar es Salaam.
Usajili wa wachezaji hao
wawili unaimarisha zaidi Simba ambayo msimu uliopita iliyumba na kuambulia
nafasi ya tatu. Wengine ambao wameshasaini Simba mpaka sasa ni Peter Mwalyanzi
kutoka Mbeya City na Mussa Mgosi aliyekuwa Mtibwa.
0 comments:
Post a Comment