MCHEZAJI mpya wa Yanga, Deus Kaseke, alitambulishwa kwa mbwembwe jijini Dar es Salaam mapema wiki hii na kuchimba mkwara, lakini kikubwa zaidi akanyoosha juu jezi namba nne ambayo ndiyo atakuwa anavaa.
Wakati huo mwenye jezi hiyo ambaye ni Rajab
Zahir alikuwa sehemu anamchabo tu kiaina, baadaye akaibuka bwana.
Rajab amelianzisha baada ya kuwaambia
mabosi wake waliotoa jezi namba 4 na kumpa Kaseke kuwa wamechemsha kwani hiyo
ni namba yake na hatakubali kunyang’anywa kirahisi.
Zahir alisema, hakubaliani na kitendo hicho
na kwamba jezi namba nne ataitumia yeye kwa sababu ni mchezaji halali wa klabu
hiyo na bado ana mkataba wa mwaka mmoja, Kaseke wamtafutie nyingine.
Akizungumza na Mwanaspoti, Zahir alisema:
“Hata kama Kaseke ametambulishwa kuwa atavaa jezi namba nne, nitakayevaa ni
mimi, yeye wamtafutie nyingine. Mimi bado mchezaji halali wa Yanga na nina
mkataba wa mwaka mmoja mbele, hivyo mengine yanayoendelea siyajui, lakini
kuhusu jezi, Kaseke wamtafutie nyingine.”
Mwanzoni mwa wiki hii, Yanga ilimsainisha
Kaseke na kumtambulisha kwa mashabiki wake kuwa atatumia jezi namba 4 msimu
ujao kama aliyokuwa anaitumia alipokuwa Mbeya City.
Awali, uongozi wa Yanga kupitia kwa msemaji
wake, Jerry Muro, ulisema umempa Kaseke jezi namba hiyo kwa sababu
mkataba wa Zahir umemalizika na klabu iko kwenye mazungumzo na mchezaji huyo
kwa ajili ya makubaliano ya msimu ujao.
Habari za ndani zinadai kwamba Yanga
wanafikiria kumwacha au kumtoa kwa mkopo Rajab ingawa bado hawajataka kuiweka
wazi.
Kaseke amtisha Msuva
Kaseke amemshtua mfungaji bora wa Ligi Kuu
Bara, Simon Msuva, anayemkuta klabuni hapo na kumwambia kwamba hamwogopi hata
kidogo na kwamba atakomaa mpaka kieleweke.
Kaseke ambaye alisaini Yanga huku akiwindwa
na Simba, alisema hali hiyo haitamvimbisha kichwa na kwamba Yanga inasifika
kuwa na viungo wengi, lakini hatishiki na atapambana hadi kitaeleweka na
akasisitiza Yanga itamfanya awe bora zaidi kikubwa apate ushirikino.
Kaseke aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja
akitokea Mbeya City, alisema atakula sahani moja kwa kupambana na wakali kama
Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Geofrey Mwashiuya, Salum Telela, Hassan Dilunga
na wengine watakaosajiliwa mpaka kieleweke.
0 comments:
Post a Comment