Kwa mujibu wa taarifa
zilizotolewa kwenye Gazeti la Lusaka Times la Zambia, imeelezwa kuwa Tanzania
inatakiwa kutafuta suluhisho la kudumu la kudhibiti ajali zinazosababishwa na
malori ya Tanzania wanayokwenda nchini humo.
Likikariri ripoti iliyotolewa
na Kikosi cha Usalama Barabarani cha Zambia mwezi huu, gazeti hilo limesema
katika ajali hizo 227, ajali 37 zilipoteza maisha ya watu 42.
“Kati ya ajali hizo waliopata
majeraha makubwa walikuwa 51, wenye majeraha madogo walikuwa 59 huku ajali 133
zilisababisha uharibifu wa magari na mali,” inasema ripoti hiyo.
Ripoti hiyo ilitaja sababu
kubwa ya ajali hizo kuwa ni mwendo kasi, vizuizi barabarani, uchovu wa safari
ambao umekuwa ukisababisha baadhi ya madereva kuegesha malori yao vibaya na
kusababisha madhara kwa watumiaji wengine wa barabara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala
wa Usafirishaji na Usalama Barabarani (RTSA) Zambia, Zindaba Soko akizungumza
katika mkutano uliomkutanisha na Mkurugenzi wa Usafirishaji kutoka Mamlaka ya
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini Tanzania (Sumatra), Leo Ngowi mjini Ndola
Zambia, alisema Serikali ya nchi hiyo itaondoa vikwazo barabarani ambavyo
vimekuwa vikisababisha ajali.
Mkurugenzi huyo alisema iwapo
nchi za Kusini mwa Afrika zitatekeleza utaratibu wa kuondoa urasimu utasaidia
kupunguza muda wa kukaa mipakani, kupunguza gharama za kufanya biashara na
kufanya safari nyingi kuliko ilivyo sasa kama pia watazingatia sheria za
usalama barabarani.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi (SACP), Johansen Kahatano kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani
akizungumzia suala hilo alisema Polisi ilituma mwakilishi katika mkutano huo
nchini Zambia ambapo walipata taarifa za ajali hizo.
Kahatano alisema Serikali
ilipendekeza madereva wenye leseni daraja E wasome kila wanapotaka kupata
daraja C, pia madereva wote wakasome kila baada ya miaka mitatu, lakini suala
halikuwezekana baada ya kupingwa na madereva.
0 comments:
Post a Comment