Wingi wa rasilimali hizo za
thamani duniani umekuwa ukiwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa nchi ni tajiri
lakini unapoingia kwenye uhalisia, utajiri huo haulisukumi taifa kumea vizuri
kiuchumi.
Je, tatizo ni nini? Kuna
mipango gani ya kukabiliana na hali hiyo? Haya ni maswali ambayo yamekuwa
yakiulizwa na wengi na makala hii inakusudia kuyajibu.
Arusha na moja ya mikoa
nchini ambao kuna uchimbaji wa aina nyingi za madini. Moja ya madini yanayoupa
sifa kubwa mkoa huu ni madini ya Tanzanite ambayo hayapatikani eneo jingine
popote duniani.
Biashara kubwa ya madini hayo
ipo katika Jiji la Arusha na kuna mitaa, ambayo ni kawaida kukuta vijana,
wakiwa wamekaa kando ya barabara wakichonga madini na kuuza. Mitaa hiyo ipo
katikati ya Jiji la Arusha kama vile Barabara ya Pangani, jengo la Chama cha
Wafanyakazi Arusha (Ottu) na Mtaa wa St Thomas.
Katika mitaa hii, utakuta
vijana wengi wakiwa na viti na meza ndogo wakichonga madini na wengine wakiuza.
Mbali na Tanzanite, pia kuna aina nyingine madini kama vile saphire, spinel,
tourmaline, sperssatite na aquamarine. Miongoni mwa madini hayo yapo
yanayochimbwa mikoa ya jirani.
Kuuzwa holela kwa madini
kunatajwa ndiyo kunasababisha madini mengi kutoroshwa na kuvuka mipaka kuingia
nchi mbalimbali ambazo huziuza kwenye soko la dunia. Aina hii ya biashara
hulikosesha taifa mapato na isitoshe hata wachimbaji na wafanyabiashara hiyo
hapa nchini hupata faida kidogo tofauti na ingekuwa wangepeleka wenyewe kwenye
soko la dunia.
Kwa mfano ripoti ya mwaka
2013 inaonyesha kuwa uuzaji wa madini ya Tanzanite uliingizia Tanzania Dola 38
tu za Marekani huku nchi zinazopata madini hayo kwa njia ya panya, zikijipatia
mapato makubwa. Kulingana na ripoti hiyo, katika mwaka huo, Tanzanite
iliingizia Kenya Dola 100 milioni na India Dola 300 milioni.
Tanzania yazinduka
Kwa kutambua namna inavyopoteza
mapato na nchi kutofaidika kikamilifu na madini yake, Serikali imeamua kuweka
mkakati ambao utaziba mianya ya utoroshaji wa madini nchini. Ili kuifanya
biashara ya madini ya vito, kutambulika kisheria na kuinufaisha Serikali katika
kukusanya kodi mipango imeanza kujengwa kituo cha kukata, kusanifu na kuuza
madini Arusha.
Kituo hiki, kinakuwa cha
kimataifa, ambacho kitakusanya wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite wa ndani
na nje ya nchi kukaa pamoja kufanya biashara halali.
Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene anasema kituo hiki, kitajengwa na Serikali kwa kushirikiana na
Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC).
0 comments:
Post a Comment