Alitoa kauli hiyo Dar es
Salaam jana alipotoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kutungwa sheria
hiyo mpya na Bunge Machi mwaka huu.
Dk. Chuwa alisema kuanzishwa
kwa sheria hiyo kunalenga kutoa mwongozo kwa taasisi za Serikali na mashirika
mbalimbali yanayotoa takwimu nchini yaweze kuendesha shughuli za ukusanyaji na
usambazaji wa takwimu kwa kuzingatia sheria hiyo mpya.
“Sheria hii hailengi kuondoa uhuru wa taasisi nyingine za utafiti kufanya kazi zao, taasisi zote za utafiti zinazotambulika katika sheria zitaendelea kuwa huru katika kufanya utafiti kwa mujibu wa taratibu zao mradi tu zinafuata sheria iliyopo,” alisema Dk. Chuwa.
“Sheria hii hailengi kuondoa uhuru wa taasisi nyingine za utafiti kufanya kazi zao, taasisi zote za utafiti zinazotambulika katika sheria zitaendelea kuwa huru katika kufanya utafiti kwa mujibu wa taratibu zao mradi tu zinafuata sheria iliyopo,” alisema Dk. Chuwa.
Alisema mbali na sheria
kuanisha kuwa takwimu rasmi ni zile zitakazotolewa na Serikali kwa maana
Wizara, Idara na taasisi zake kulingana na vigezo vilivyowekwa na kamisheni ya
Umoja wa Mataifa ya Takwimu ambayo inatoa msisitizo wa takwimu zinazotolewa na
taasisi au mtu binafsi kutambuliwa.
“Kifungu cha 20 cha sheria
hii kinaeleza kuwa takwimu zinazotolewa na taasisi nje ya Serikali kwa kukidhi
vigezo vya takwimu vilivyowekwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikiwamo
kuzingatia mbinu za kukokotoa takwimu zitatambuliwa kuwa rasmi na zitatumika
katika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi,” alisema Dk. Chuwa.
Ufafanuzi huo umetolewa siku
chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kutia saini Sheria ya Takwimu na Sheria ya
Makosa ya Mtandaoni za 2015.
Hata hivyo, gazeti la The
Washington Post la Marekani limekosoa hatua hiyo likidai kuwa itakwenda kinyume
na uwazi na utawala bora.
Katika toleo la Mei 15 la
gazeti hilo, mwandishi Karen Attiah ambaye ni mchambuzi na mhariri msaidizi wa
kitengo cha dijiti ameitaka Serikali ya Marekani na mashirika ya maendeleo hasa
Benki ya Dunia kuimulika Tanzania kwa kupitisha sheria zinazokandamiza uhuru wa
habari.


0 comments:
Post a Comment