Image
Image

News Alert: Waendesha bodaboda zaidi ya 50 wafunga barabara na kutuhumu vikundi vya ulinzi shirikishi kuchukua rushwa.


Zaidi ya vijana 50 wakiwa na msururu wa pikipiki maarufu kama (Bodaboda)wamefunga lango la ofisi za kutuo cha urushaji wa matangazo nchini Tanzania ITV/Radio one  wakilalamikia uonevu wanao fanyiwa na vikundi vinavyo jiita Polisi jamii,Tambaza na ulinzi shirikishi pindi wawapo katika majukumu yao yakazi na kutozwa zaidi ya shilingi elfu hamsini hadi laki moja kwa madai ya faini ya kukiuka sheria za usalama bara barani jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na Tambarare Halisi wakati wakiwasilisha kilio chao kwa lengo la kutafutiwa ufumbuzi na viongozi wanaohusika pindi watakapo iona habari hiyo vijana hao ambao wametoka maeneo ya kawe,tangibovu na maeneo jirani wamesema wameunganisha nguvu ili kupinga vitendo wanavyo fanyiwa na vikundi hivyo kwani imekuwa nikama desturi hali ambayo wamekuwa wakinyanyasika na huku wakiwa na familia zinazo wategemea.

Wamesema kuwa wao kama waendesha bodaboda hawana ugomvi wa aina yeyote na askari wa usalama barabarani kwa kuwa endapo mtu atakuwa kakiuka sheria za usalama bara barani basi watapigwa faini inayo landanda na kosa lenyewe tofauti na vikundi ambavyo havina sare wala vitambulisho vinavyoibuka kwa lengo la kujitafutia maslahi binafsi katika mgongo wao bila hata huruma ya aina yeyote.

Makundi hayo yamekuwa mara kadhaa yakiwavizia wakati wakiwa kwenye foleni na hivyo kuwanyang”anya funguo wakiwataka wawapatie kiasi cha fedha wanazo taka wao,hali ambayo waendesha bodaboda wanadai kuwa wanaendesha pikipiki hizo kimachale kwani wanapo waona wanakimbia ndipo wakati mwingine hujikuta wakipata ajali zisizo na sababu kwa kukwepa kulipa fedha ambazo hazijulikani zina kwenda wapi.

Kufuatia malalamiko hayo ya waendesha Bodaboda Tambarare ikafanikiwa kuzungumza na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kiondondoni kamanda Awadhi Haji kwa lengo la kutaka kufahamu kwamba je malalamiko haya wanayajua ama la?. Na kama wanayajua zipi juhudi walizofanya kutatua hili?.

Kamanda Awadhi amesema kuwa kikosi chake kipo safi katika kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria na hivyo askari wake wakiwa wamevalia sare kila wawapo sehemu ya kazi na hivyokusema kuwa”Kwa malalamiko haya kuna kunasababu na haja ya madereva kufika ofisini kwangu na kutoa ushirikiano mzuri ili kuweza kukomesha makundi ambayo yanalichafulia heshima jeshi la polisi kwa kupokea rushwa kinyume na taratibu na hivyo sheria kufuata mkondo wake.

Bwana.Kalos Mbwalo ni mwakilishi/mwenyekiti asiye rasmi aliyechaguliwa na wenzie ili kuweza kufikisha kiliochao,ambapo amesema”Sisi tuliofika hapa niwachache ila tunawakilisha wenzetu wengine ambao wapo maeneo mbali mbali ya mjii huu wa Dar es Salaam wakipatwa na kadhia hii ya kutoa rushwa pasipo kujulikana fedha zina kwenda wapi”Alisema Mbwalo.

Amesema wao kipo kitu wanacho kishangaa mno hasa katika taifa hili ambalo hiki ni kipindi cha uchaguzi kwa namna kunavyoonekana kuwepo kama na ubaguzi kutokana na kwamba ingawa serikali imekataza pikipiki hizo kuingia mjini lakini wanashangaa kwamba mbona wapo waendesha bodaboda mjini na wanaingia maeneo mengine kupeleka abiria sasa Je mbona wao wakiingia mjini hukumbana na vikwazo vingi,kwani hizo piki piki zina mkono wa watu wakubwa(Vigogo)ama tafsiri yake nini haswa jambo hilo linawapa kigugumizi kikubwa.

Kutokana na changamoto wanazokutana nazo hizo wameelekeza kilio chao kwa kikosi cha usalama barabarani pamoja serikali yake kwa ujumla kuangalia namna ya kuwasaidia kwani kazi wanayoifanya ni yakujiingizia kipato pamoja na familia zao,na kutokana na ajira kuwa ngumu wamejiajiri wenyewe lakini wachache wanawanyonya kwa hata kidogo wanacho kipata jambo ambalo linawaumiza kwa kiasi kikubwa.

Wanadai kuwa katika kazi hiyo ya kuendesha boda boda kwa wao usalama ni hafifu kufuatia siku za nyuma walikuwa wana kabwa na kuuawa na pikipiki zao kuibiwa,na wanaofanya shughuli hiyo ni watu wanao tumia magari ya NOAH ambayo wao wenyewe wanayaogopa kwani yamekuwa yakifanya shughuli za kihalifu,kwani wanapo tekeleza jaribio la wizi kwa waendesha boda boda huwapiga na kutupwa nje na pikipiki kupakiwa kwenye gari hiyo na kuondoka nayo hivyo jeshi liangalie kwa umakini wasidhani bodaboda tu ndio wahalifu mbinu za uhalifu zimebadilika.

Hata hivyo wamesema kwamba kutokana na matatizo hayo sasa wapo makini kuangalia kiongozi atakaye faa na kutatua matatizo yao na huyo ndiye watakaye mpatia na kumpigia kura hapo Octoba mwaka huu katika uchaguzi mkuu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment