Bwana NKURUNZIZA ambaye
amekabiliwa na wiki za maandamano kupinga uamuzi wake wa kugombea muhula wa
tatu na jaribio la mpinduzi alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza katika mji
mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura hapo jana.
Lakini katika kauli yake hakugusa
mambo ya maandamano na jaribio la mapinduzi na badala yake alichosema ni kwamba
mawazo yake zaidi yako kwenye tishio la kikundi cha al-Shabaab kwa nchi yake.
Burundi ni miongoni nchi za
wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika huko Somalia ambazo zimekuwa
zinalengwa kwa mashambulio na kikundi cha al-Shabaab.


0 comments:
Post a Comment