Image
Image

News Alert: Wananchi na viongozi wa dini Wilayani Karatu Mkoani Arusha wamewa lalamikia wanasiasa kugeuza nyumba za ibada kuwa majukwaa ya siasa.


Wananchi na viongozi wa dini Wilayani Karatu Mkoani Arusha  wamewa lalamikia  wanasiasa   kugeuza  nyumba  za  ibada kuwa  majukwaa  ya  siasa na wameiomba Tume   ya  Taifa ya  Uchaguzi  ku weka utaratibu wa  kudhibiti  hali hiyo kabla haijaota  mizizi .
Wakizung umza katika uzinduzi wa Kanisa  Katoliki  la Parokia ya Kitete   Wilayani Karatu ,wananchi  na  viongozi  hao  akiwemo   Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Musoma   Bwana   MICHAEL MDONGAZILA  wamesema  wanasiasa wanaweza kufanya kampeni zao na zikaenda vizuri   bila kuyahusisha madhehebu ya dini hivyo hakuna sababu ya wanasiasa kutumia nyumba za ibada .
Askofu  MICHAEL  amesema licha ya  kuwepo  kwa   u husiano   wa dini  na  siasa, kila kimoja kina taratibu  zake  na ni  vyema  zikafuatwa  na  kulindw a,  kwani  uzoefu  unaon es ha  kuwa  maeneo yote ambayo  dini na  siasa  zimechangan ywa amani  imetoweka.
Wananchi  hao  am bao asilimia kubwa ni wakulima  wametumia  hafla hiyo  kueleza kero ya  ubovu wa miundombinu ya barabara  wakidai   kuwa  nyingi  hazipitiki hasa wakati  huu wa mvua jambo  linalosababisha  washindwe  kusafiri  kutoka  eneo moja  hadi  jingine  kutafuta  mahitaji yao yakiwemo  ya chakula .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment