Meneja wa shirikisho hilo Mkoani Kigoma,JANE CHAGIE amesema tayari timu ya watendaji wameshakwenda
Kijijini Kagunga wakiwa na mahema kwa ajili ya waomba hifadhi hao
kujihifadhi, dawa ya kusafisha maji pamoja
na watu wanaoshughulikia uchimbaji vyoo.
Akizungumzia suala la uchimbaji
vyoo amesema,wamekabiliwa na tatizo kubwa la mahali pa kuchimba vyoo kutokana
na sehemu kubwa ya eneo kuwa la Milima yenye mawe na
idadi kubwa ya watu ikiwa kandokando ya Ziwa Tanganyika.
Kijiji cha Kagunga kinakadiriwa
kuwa na zaidi ya waomba hifadhi Elfu -90
wanaosubiri kusafirishwa kwenda kambi ya wakimbizi Mtabila Wilayani
Kasulu, hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira katika kijiji hicho kutokana
na huduma duni za afya na jamii.
0 comments:
Post a Comment