Akisoma shitaka mbele ya hakimu mkazi Ivan Msaki, mwendesha mashataka wa polisi Aminata Mazengo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo may 20 kinyume na kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu nahakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa lenyewe na kuwa mtuhumiwa yuko chini ya miaka 18 hivyo kuwakilishwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi
juni 10 mwaka huu itakapo tajwa tena mahakani hapo .
Katika hali isiyo ya kawaida
ndugu wa marehemu Ediga Mafwere kwa hasira amempiga ngumi mtuhumiwa muda
mfupi baada ya kutoka mahakamani mbele ya maafisa wa jeshi la polisi
na ustawi wa jamii ambapo naye alijikuta katika mikono
ya jeshi la polisi na kufungwa pingu ambapo anashikiliwa kwa mahojiano
zaidi.
Akizungumza juu ya uhakika wa
usalama wa msichana Judith Chomile afisa ustawi wa jamii manispaa ya Morogoro
Jasmin Masenge amesema msichana huyo atakuwa katika mikono salama chini
ya uangalizi wa kitengo cha ustawi wa jamii pamoja na jeshi la polisi kitengo
cha dawati lajinsia na watoto hadi kesi inayomkabili itakapotolewa hukumu.


0 comments:
Post a Comment