Image
Image

Uchaguzi mkuu wa urais wa shirikisho la soka la Dunia-Fifa utafanyika ijumaa hii.


Uchaguzi mkuu wa urais wa shirikisho la soka la Dunia-Fifa utafanyika ijumaa hii pamoja na viongozi 7 wa shirikisho hilo kushitakiwa kwa kosa la kupokea rushwa ya dola milioni 150.
Makamu wa rais wa shirikisho hilo Jeffrrey Webb ni kati ya waliokamatwa kwa kosa la kupokea rushwa pamoja na viongozi wengine wa juu 6.
Uchunguzi mwingine umeshaanza kufanyawa kuhusu namna nchi zitakazokuwa wenyeji wa kombe la dunia kwa mwaka 2018 na 2022 zilivyopewa heshima hiyo.
Lakini Fifa imesisitiza kuwa urus na Qatar ndio wenyeji wa kombe ladunia kwa mwaka 2018 na 2022 kwani wanaamini uchunguzi huo hautabaini baya lolote.
Na timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliiers imetinga fainali za ligi ya mpira wa kikapu ya marekani baada ya kuwachakaza Atlanta Hawks kwa vikapu 118-88.
Kwa mara nyingine tena Lebron James aliibeba Cavs akimaliza na vikapu 23 kuokoa mipira mara 9 na kutoa pasi za mwisho 7 na kisha kuwa mshangiliaji mkuu kwa karibu robo nzima ya mwisho ya mchezo.
Cavalliers sasa wanasubiri mshindi kati ya Golden State Warriors na Houston Rockets.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment