Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya
Mrisho Kikwete tayari ameshasaini sheria yenye utata ya makosa ya mtandao.
Sheria hiyo itaanza kutumika muda wowote kuanzia
sasa.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amesema hayo leo wakati akizungumzia masuala
mbalimbali yanayohusu sheria hiyo ambayo kupitishwa kwake kumesababisha
malalamiko mengi kutoka kwa wadau kuwa itaminya uhuru wa habari, kuingilia
faragha pamoja na uhuru wa watu kuwasiliana.
Ufuatao hapa chini ni uchambuzi kidogo kuhusu baadhi
ya vipengele vilivyozua utata katika muswada huu uliokuwa umetolewa.
1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver)
anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa
jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la
jinai).
2. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu
ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi
kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).
3. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza
kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au
kulipa milioni 30; (Mfano: mtu kaposti picha yake ambayo sio ya ponografia
lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!)
4. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi
ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo
kisichopungua mwaka mmoja?
5 Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na
ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza
kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. (Mfano: unapofuta ‘status’
zako za WhatsApp, unaweza shitakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta
na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.)
6. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini
anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye
email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda
ya Mahakama.
7. Serikali kupitia Waziri husika ndio ina mamlaka
ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha.
0 comments:
Post a Comment