Image
Image

News Alert:Mafuriko yaua 8 kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.


Watu wanane wamekufa hadi sasa Jijini Dar es Salaam kutokana na mafuriko ambayo yamewakumba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam  kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,   Bwana  SAID MECK SADIQ amethibitisha kutokea vifo hivyo na kuongeza kuwa madaraja kadhaa yamebomolewa na maji maeneo mbalimbali ya jiji hilo na kusema watoto ni waathirika wakubwa kwa kusombwa na maji.

Akizungumza na Tambarare Halisi kwa njia ya Simu  Bwana SADIQ  amesema mbali na vifo hivyo , baadhi ya wak azi wa maeneo mbalimbali hawana  makazi ,   baada ya nyumba zao kujaa maji na kulazimika kuhifadhiwa na wasamaria wema  na  wengine wakijihifadhi katika vituo  vya abiria katika Barabara ya Morogoro .

Amesema  wananchi wa maeneo mbalimbali  ya jiji  haw ana mawasiliano ya barabara,  baada ya   madaraja kusombwa na maji  na kusema  vikosi vya u o ko aji   vinaendelea na juhu di za kuokoa watu katika maeneo   mbalimbali .

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam ameyataja m aeneo yali yo athirika zaidi  kuwa  ni pamoja na Kinondoni Mkwajuni ambapo watu wapatao kumi na  mbili wameoklewa na kikosii cha  Zima Moto, maeneo ya Kigogo ,  hasa wanaoishi karibu na Mto Ng ' ombe na Mto Msimbazi, maeneo ya Boko na maeneo ya Goba .

Amesema Shule ya Msingi Jangwani Beach imefungwa kdutokana na vyoo vyake kubomoka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment