Katibu wa chama cha wauguzi tanzania ( TANNA ) tawi
la hospitali ya rufaa Bugando Lydia Chuwa
ametoa ombi hilo wakati akisoma risala
ya siku ya wauguzi duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka kwa ajili ya
kukumbuka siku aliyozaliwa muasisi wa taaluma ya uuguzi duniani Bi. Florence Nightingali ambapo kaulimbiu ya mwaka huu
inasema wauguzi ni nguvu ya mabadiliko, huduma bora gharama nafuu.
Akizungumza na wauguzi hao mkurugenzi mkuu wa
hospitali ya rufaa bugando Prof. Dk. Kien Mteta amewataka wauguzi kuhakikisha
wanatoa huduma nzuri kwa wagonjwa ili ziweze kuleta matokeo chanya katika
taswira ya uuguzi, ambapo pia amewashauri kujiendeleza kimasomo na kuzingatia
maadili katika kutoa huduma kwa wateja na hivyo kuwa nguvu ya mabadiliko na
raslimali muhimu ya afya.
Baadhi ya wauguzi wamesema wataendelea kuzingatia
viapo vyao walivyoviapa wakati wanahitimu taaluma ya uuguzi licha ya kufanya
kazi katika mazingira yenye changamoto nyingi.
Kisha ukawadia wakati wa mkurugenzi wa huduma za
uuguzi katika hospitali hiyo Bi. Mashauri kuwaongoza wauguzi hao 434 katika
tendo la kuwasha mishumaa na kurudia kiapo chao.




0 comments:
Post a Comment