Wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashirika wamelaani jaribio la mapinduzi yaliyotaka kufanyika nchini burundi huku
wakitaka utawala wa sheria kwa kuheshimu katiba na makubaliano ya arusha pamoja na kusogezwa mbele.
Akisoma maazimio ya mkutano huo
mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais Jakaya Kikwete amesema wanatambua hali ya
kisasa iliyotokea burundi na hivyo wanasisitiza makubaliano ya Arusha
yaheshimiwe.
Mkutano huo umekubaliana kwa
pamoja uchaguzi wa burundi usogezwe mbele hadi hali ya siasa itakapotengemaa.
Tofauti na matarajio ya wengi
Rais Pierre Nkurunziza hakuweza kuhudhuria mkutano huo licha yakuwepo taarifa
kuwa aliwasili jijini Dar es Salaam.




0 comments:
Post a Comment