Kikao Kikiwa kinaendelea jana usiku.
Mwenyekiti wa Vuguvugu kutoka nchini Burundi Bw. Mugwengezo Chauvineau akiongea
na waandishi wa Habari Serena Hotel Dar jana usiku.
Dr. Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa Nchini Burundi, Akiongea na waandishi wa Habari jana usiku .
Dr. Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa Nchini Burundi, Akiongea na waandishi wa Habari jana usiku .
Mwenyekiti wa vuguvugu za Maandamano Burundi kwa Mara ya kwanza amefika Nchini
Tanzania ili kuweza kushuhudia Mkutano wa Dharula kati ya viongozi watano wa
Jumuia ya Afrika Mashariki kuhusu nchi ya Burundi ambayo sasa imeingia katika
machafuko baada ya Rais aliyepo Madarakani kutaka kuongeza muda wake.
Akiongea na Waandishi wa Habari usiku huu Mkuu huyo wa vuguvugu wa Burundi amesema kuwa wananchi hawaridhiki na Rais wao kuendelea kuwa madarakani ambapo hata sheria na katiba hairuhusu na pia sasa ni wiki ya tatu ambapo wananchi wanaendelea kupinga Rais kuendelea kuwania kwa Muhura wa Tatu.

Amezungumzia juu ya waandamanaji baada ya wiki tatu bado wapo barabarani ambapo
wameweza kuwa ni kiungo, wameweza kuwa ni njia kwa sababu wanadai kumekuwa na
mabadiriko kuhusu Rais wao, na kuwashukuru waandamanaji hao kwa kuonesha moyo
wa uzalendo na kuwa wameweza kudhihilisha na kuwa walikuwa ni watulivu na
kutulia kungoja utekelezaji wa mambo ambayo yamezungumziwa.
Amesema kwamba anaomba vurugu hizi zipate kwisha ambapo watu zaidi ya laki
mbili wamekimbia nchi na anaomba vurugu ziishe ili wapate kurejea nchini kwao.
Pia ameiomba Jumuia ya kimatafa iweze kufuatilia kwa karibu hali inayoendelea
kwa sasa Nchini Burundi ambapo jumuia iyo tangia zamani imeweza kusimamia mambo
ya usalama nchini Burundi na amani ili Burundi iweze kufikia malengo ya Mkataba
wa amani wa Arusha na kufikia malengo ya katiba ambayo ndio uti wa mgongo wa
taifa hilo.
Kuhusu jaribio la Mapinduzi kiongozi huyo amesema hayupo Miongoni mwa wale
ambao wameandaa tukio hilo
Kuhusu jambo baya alilofanya Rais wa Burundi Kiongozi huyo amaesema kwamba ni
kuongezea Muhula wakati tayari alisha tawala kwa Miaka 10, na katika miaka hiyo
alishindwa kuweka usawa baina ya warundi, hajatekereza swala la haki za
Binadamu , aliongeza kuwa Muhura wake ni Muhura baki na Haramu hauko sambamba
na Katiba wala Sheria ya Burundi pamoja na Mkataba wa Arusha na angetekeleza
yote hayo hizi vurugu zisinge kuwepo.
Pia hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula mitatu. Pia warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena Damu inamwagika.
Pia hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula mitatu. Pia warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena Damu inamwagika.
Mwisho amewaomba Marais watano wamalize salama Mkutano na kuhakikisha maamuzi
yote yanafanyiwa kazi.
Nae Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea kuwa madarakani kwa awamu ya Tatu.
Nae Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea kuwa madarakani kwa awamu ya Tatu.

0 comments:
Post a Comment