Wakizungumza kwa masikitiko wananchi hao ambao
baadhi yao kwa sasa wamehifadhiwa katika nyumba za ibada ,shule na
wengine katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha TPC wamesema kwa sasa
wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana mali zao ikiwemo baadhi
mifugo na vyakula kuchukuliwa na maji.
Wananchi hao wameiomba serikali kuangalia uwezekano
wa kuwasaidia misaada ya haraka ya chakula na dawa kutokana kuwepo hatari
ya kupatwa na magonjwa mlipuko na malaria.
kwa upande wake diwani wa kata ya TPC Bw.Rojas
Mmari na afisa utala mkuu wa kiwanda cha kuzalisha sukari TPC BW.JAFARY ALLY wamesema
kwa takribani miaka 30 kata hiyo haijawahi kukubwa na mafuko makubwa kamahayo
na kwamba wananchi hao wanahitaji msaada wa haraka wa vyakula nguo na
vyandarua.
Kufuatia tatizo hilo mbunge wa viti maalum chadema
mkoa wa kilimanjaro Mh.Lucy Owenya ametembelea wananchi hao na kuona adha
waliyoipata na kutoa msaada wa chakula ambapo ameitaka serikali ya
wilaya kuchukua hatua za haraka za kusaidia wananchi hao.
0 comments:
Post a Comment