Rais wa msumbiji Mh. Filepe Jacinto Nyussi
leo amelihutubia bunge la jamhuri ya Muugano wa Tanzania Mjini Dodoma na kusisitiza
ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji tangu enzi za harakati za kutafuta uhuru wa Msumbiji ambapo Tanzania
iliikuwa msaada mkubwa kwa nchi hiyo.
Rais Nyussi aliyeambatana na mwenyeji wake
Rais Jakaya Kikwete amesema Msumbiji itaendelea kuimarisha zaidi uhusiano wa
kijamii, kiuchumi na kiusalama baina ya Msumbiji na Tanzania kuelezea dhamira
yake ya kulihutibia Bunge la Tanzania siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa
rais.
Katika hotuba yake Rais Nyusi amesema
serikali yake imejitolea kuimarisha uhusiano
wa miaka mingi kati yake na Tanzania na hivyo angependa kuwaalika
wawakilishi wa Bunge la Tanzania nchini Msumbiji kusudi kuweza kujifunza mambo
mbali mbali.
Kwa upande wake Spika wa Bunge nchini Anne
Makinda amempongeza Rais Nyusi kuchaguliwa na watu wa Msumbiji kuwaongoza na hivyo kuchukua uamuzi wakuja nchini kwa mara
ya kwanza tangu achaguliwe na kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Kwaniaba ya wabunge wote Spika Makinda
amemshukuru Rais Nyusi na kusema kuwa tangu
ya uongozi wa waasisi wa mataifa haya,wamechukua hatua madhubuti za kukuza
uhusiano, na ziara yake hapa nchini ni kielelezo tosha kuwa mabunge ya nchi
zetu mbili yamekuwa na uhusiano wa muda mrefu, kupitia vyama vya mabunge na
wamekuwa wakishiriki katika semina na ziara mbalimbali za mafunzo,hivyo wanaendelea
kukuza uhusiano huu.
Makinda amesema ujio wa Rais
Nyusi umekuwa na faraja nzuri kwa taifa la Tanzania hivyo wamempatia zawadi ya picha ya bunge
la Jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati wa picha ya pamoja.


0 comments:
Post a Comment