Hali mbaya ya ukosefu wa amani nchini Yemen
iliyosababishwa na mashambulio ya kinyama ya Saudi Arabia katika nchi hiyo,
yamepelekea maelfu ya wakimbizi wa Kisomali waliokuwa nchini humo kurejea kwao.
Nicholas Kay, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa
nchini Somalia ametangaza kuwa, wakimbizi elfu saba wa Somalia waliokuwa nchini
Yemen wamerejea nchini kwao baada ya usalama nchini Yemen kuzidi kuwa
mbaya.
Nicholas Kay amesema hayo katika hotuba yake kwenye
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kubainisha kwamba, kuna haja ya kuweko
usimamizi wa karibu kwa wakimbizi hao wanaorejea nchini Somalia.
Aidha amesema, kuna ulazima wa kuchukuliwa hatua za
kukabiliana na tishio la kundi la kigaidi la al-Shabab. Ripoti za Umoja wa
Mataifa zinaonesha kuwa, kuna wakimbizi laki mbili na nusu wa Somalia nchini
Yemen.


0 comments:
Post a Comment